Tuesday, December 23, 2014

CCT RUCO YATEMBELEA WAHITAJI

CCT RUCO YATEMBELEA WAHITAJI


Uongozi wa CCT RUCO kwa kushirikiana na washarika ulitembelea Shule ya Msingi ya watu wenye matatizo ya kusikia ( Shule ya msingi viziwi Iringa) iliyopo maeneo ya Mtwivira na kupata nafasi ya kupeleka mahitaji mbali mbali kwa wanafunzi wa shule ile. Wana CCT wakiongozwa na Mchungaji wa Usharika wa CCT RUCO, Madam Angel, na Viongozi wa usharika walipata nafasi ya kushinda pamoja na watoto wale, na kujifunza mambo mbalimbali yanayofanyika katika shule ile huku wengine wakipata nafasi ya kujifunza lugha ya mawasiliano inayotumiwa na watoto wenye ulemavu wa kusikia. 

Kivutio kikubwa katika ziara hiyo kilikuwa ni mechi ya mpira wa miguu iliyochezwa kati ya timu ya mpira wa miguu kati ya CCT RUCO na Wanafunzi shule msingi viziwi Iringa ambapo walitoshana nguvu kwa kutoka uwanjani kwa gori 1 kwa 1. Mechi hiyo ilikuwa ya kusisimua huku timu ya mpira wa miguu CCT ikikutana na ufundi wa hali ya juu toka kwa wachezaji chipukizi wa shule ya Viziwi Iringa.

Aidha katika ziara hiyo ilielezwa na Mwalimu mkuu wa shule kuwa shule inao wanafunzi 110 toka darasa la kwanza mpaka la saba na kuwa katika shule ile pamoja na kupokea na watoto wenye ulemavu wa kusikia pia wanao watoto enye matatizo pacha yaani wasiosikia na kuona na kuwa shule imegawa madarasa katika makundi mbali mbali kulingana na uwezo wa watoto na kuwa lipo daras la ujasiliamali ambapo watoto hundishwa kazi za mikono bila kujali hli zao ili waweze kujitegemea siku za baadae. Funzo kubwa kutoka na ziara ile ni kuwa hakika Mungu amewatia huruma walimu wa shule ile na kuwa wanafanya kazi kwa moyo wa kujituma maana changamoto walizozieleza kuwakabili ni ngumu sana. Aidha mkuu wa shule alieleza kuwa shule ile inapokea wanafunzi toka sehemu tofautitofauti za nchi hii.
FUATIIA MATUKIO YA PICHA










Timu ya mpira wa miguu ya CCT










Mwalimu wa lugha ya mawasiliano


















Mwalimu Mkuu akitoa shukrani baada ya mechi




Mwalimu Mkuu wa shule akitoa maeleke





















Mwalimu wa shule ya msingi viziwi Iringa





















Dada Mkuu wa shule


Moja ya kazi za mikono zinazofanywa na wanafunzi 





















No comments:

Post a Comment