Sunday, October 19, 2014

UZINDUZI- VYOMBO VYA MUZIKI ( DRUM) CCT RUCO


Kamati ya ununuzi wa vyombo vya muziki inamshukuru Mungu kwa kutimiza jukumu la ununuzi wa vyombo vya Muziki kama lilivokuwa lengo lao la kununua drum pamoja na Mike zake. Kwa mujibu wa mwenyekiti kamati imefanikiwa kununua vyombo hivyo katika muda waliojiwekea .

TAARIFA YA KAMATI

Awali ya yote tunapenda kumshukuru Mungu kwa kutupa uhai nia, na nguvu za kumtumikia kwa ajili ya utukufu wake.  Pia tunapenda kuwashukuru ninyi wasaharika kwa namna mlivyojitoa na kuchangia katika kufanikisha lengo la kamati hii. Kamati hii iliundwa mnamo taarehe 17/05/2014 ikiwa na wajumbe 13 Kamati iliweka lengo la kupata sh 1,200,000/= na wana KAMATI walihaidi kutoa sh 50,000/= kila mmoja ili kufanikisha lengo la kupata sh 650,000/= na kuweka  mikakati zaidi ya kutimiza lengo.

MAKUSANYO YALIYOPAATIKANA

1. Wanakamati walichangia                                                               495,000/=
2. Minada Kanisani                                                                              702,000/=
3. Shukrani za washarika zilizoelekezwa kwenye kamati         203,000/=
                                                                                               JUMLA   1400,000/=



                       Mwenyekiti wa kamati ya ununuzi wa vyombo akisoma ripoti ya kamati

                                                             UNUNUZI WA NGOMA

Kwa kuwa lengo la kanisa lilikuwa ni kupata sh 1200,000/= na likazidi na kupatikana sh 1400,000/= Kamati ilipanga kununua ngoma za sh 1200,000/= na kuongeza vifaa vingine kama mike, stendi, na nyaya zake  kamati iliteua wajumbe watatu kwa ajili ya ununuzi wa vifaa hivyo.

Wajumbe waliokwenda kununua walikuta mabadiliko ya bei kinyume na ilivotegemewa na waliwashirikisha wajumbe wengine na wakaamua kununua ngoma zenye ubora zaidi zenye thamani ya sh 1400,000/= ambazo zitakabidhiwa leo kwa usharika.

Mwisho tunamshukuru Mungu kwa kutuwezesha kutimiza lengo letu.
'' TAZAMA JINSI ILIVYO VEMA NA KUMPENDEZA NDUGU WAKAE PAMOJA KWA UMOJA''( Zab: 133). Bwana anasema " MSIFUNI KWA MAVUNO NA KWA BARAGUMU MSIFUNI KWA KINANDA NA KWA KINUBI.( Zab: 150)

                                      WAJUMBE WA KAMATI YA UNUNUZI WA VYOMBO
                               WAJUMBE WA KAMATI YA UNUNUZI WA VYOMBO
                                WAJUMBE WA KAMATI YA UNUNUZI WA VYOMBO

                               WAJUMBE WA KAMATI YA UNUNUZI WA VYOMBO


                                   WAJUMBE WA KAMATI YA UNUNUZI WA VYOMBO


                           WAJUMBE WA KAMATI YA UNUNUZI WA VYOMBO             


                           PICHA: WAJUMBE WA KAMATI WAKIOMBA WAKATI WA KUKABIDHI 
                                                                      DRUM KWA KANISA










No comments:

Post a Comment