Saturday, January 19, 2013



                  Tamasha kubwa la uimbaji launguruma Ruco
Uongozi wa kwaya ya Hope ya CCT RUCO umeandaa tamasha la uimbaji lililofanyika leo tarehe 13/01/2013 katika ukumbi mkubwa wa Ruco.Tamasha hilo limepambwa na kwaya mbalimbali za manispaa ya Iringa zikiwemo Kwaya kuu kutoka chuo kikuu cha Tumaini,Youth Alive kutoka chuo kikuu cha Mkwawa,Mtakatifu Cecilia kutoka Ruco,Mlima Sinai kutoka wilolesi,TAC kutoka kanisa kuu la Anglikana,Faith kutoka Tumaini na waimbaji binafsi waliotumbuiza alikuwa ni Jackson Mustafa kutoka Ruco.Tamasha hilo liliandaa harambee ya kuichangia kwaya ya Hope kwa ajili ya maandalizi ya kutengeneza mkanda wa picha(shooting)ambayo yanatarajiwa kuanza rasmi tarehe 18/01/2013.Tamasha limefunguliwa kwa sala na Mchungaji Canon Nyagawa wa CCT RUCO.
             Baadhi ya wanakwaya ya Hope wakiwa katika picha ya pamoja baada ya tamasha hilo.
                 
Wanakwaya wa Youth Alive kutoka Mkwawa wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kutumbuiza nyimbo zao 
Kwaya ya Faith kutoka Tumaini wakitumbuiza jukwaani tamasha lilifana sana kwa picha zaidi za tukio zima bofya hapa
Askofu Joseph aongoza ibada ya kuwasimika viongozi
Askofu wa kanisa la Anglikana jimbo la Iringa aongoza ibada ya kuwasimika viongozi wapya wa CCT RUCO baada ya viongozi wa zamani kumaliza muda wao wa uongozi.
Wafuatao chini ni viongozi  wanaomaliza muda wao wakimusikiliza kwa makini Askofu Joseph.
Kutoka kulia ni Mwenyekiti,Makamu mwenyekiti,Katibu,Katibu Msaidizi na viongozi wa kamati mbalimbali.
Viongozi wanaomaliza muda wao wakiwakabidhi mishumaa viongozi wapya kama ishara ya kukabidhiana madaraka mbele ya waumini.
Uongozi wa CCT RUCO umefanya uchaguzi wa viongozi
Uongozi wa CCT RUCO umechagua viongozi wapya watakaoongoza usharika huo kwa mwaka 2013/2014 baada ya uongozi wa zamani kumaliza muda wao.Uchaguzi huo ulisimamiwa na Mchungaji Masaba kutoka AIC akisaidiana na Mchungaji Canon Nyagawa na tume ya uchaguzi iliyokuwa imeteuliwa kusimamia swala zima la uchaguzi.Kwa ujumla uchaguzi ulienda vizuri na hatimaye kuwapata viongozi ambao watalitumikia kanisa kwa mwaka 2013/2014 na wataanza kazi rasmi baada ya kuwekewa wakfu tarehe 13/01/2013.
Mchungaji Canon Nyagawa akitoa maelekezo kabla ya kuanza uchaguzi kushoto ni Mchungaji Masaba.

Wafuatao ni viongozi walioibuka kuwa washindi baada kinyanganyiro cha uchaguzi kutoka kushoto ni Victoria Magata (Mweka Hazina),Amani Ernest(Katibu Msaidizi),Peter Jacob(Katibu),Furaha Lutumo(Makamu Mwenyekiti)na Lawrence Mwamakula (Mwenyekiti)
Waimbaji wa kwaya ya Hope wakiimba kwa shangwe baada ya uchaguzi.
Kwa picha zaidi za tukio la uchaguzi tembelea page yetu ya Matukio ya picha hapo juu.

                              Malaki na Amida wameremeta 
Malaki alikuwa mjumbe wa CCT RUCO aliyehitimu masomo yake ya sayansi ya jamii katika kitivo cha elimu tarehe 30/11/2012 katika chuo kikuu cha Ruaha na akaona si vyema akaondoka peke yake aliamua kufunga pingu za maisha na Bi Amida wa Ifunda tarehe 31/11/2012 katika Usharika wa CCTRUCO kama inavyoonekana katika picha.
                                 
Malaki akimvisha pete Bi Amida na mbele yao anayeonekana ni Mchungaji Canon Nyagawa aliyewafungisha ndoa siku hiyo.                                                
 Picha zaidi za Harusi ya Bw Malaki bofya hapa
                         
                             CCTRUCO waongeza idadi ya wanachama
Uongozi wa CCTRUCO ukishirikiana na wanachama wake umefanya sherehe ya kuwakaribisha wanachama wapya ambao ni wanachuo wa mwaka wa kwanza kwa ngazi ya Astashahada,Stashahada,Shahada na shahada ya uzamili,sherehe hiyo ilitanguliwa na ibada iliyoongozwa na Mchungaji Mutta kutoka chuo kikuu cha tumaini na baadae sherehe iliyofanyika katika ukumbi wa hall D wa chuo hicho iliyoongozwa na Mgeni Rasmi ambaye alikuwa ni Mkuu wa Chuo kikuu cha Ruaha Rev Dr.Cephas Mgimwa ambaye aliwasihi wana CCT kutumia muda wao vizuri wanapokuwa chuoni waepukane na makundi yanayoweza kuwapotosha ,Na vilevile alisema wanapomheshimu mungu  wanaweza kutengeneza viongozi waliolelewa maadili ya kanisa.Mwisho Mgeni rasmi amewatakia baraka na mafanikio wanafunzi hao katika masomo yao.
Rev Dr Cephas Mgimwa akihutubia wana CCTRUCO kwenye sherehe ya kuwakaribisha mwaka wa kwanza.
                                                  


                    Salaam kutoka Uongozi wa CCT RUCO
Kwaniaba ya Uongozi wa CCT RUCO tunawakaribisha wanachuo wote baada ya mapumziko marefu na pia tunapenda kuwakaribisha wanachuo wote wa mwaka wa kwanza karibuni sana mnapokuja kuanza masomo yenu msimsahau mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema aliyetuwezesha kurudi  kuanza mwaka mpya wa masomo tukiwa wenye afya njema.Mungu awabariki na azidi kuwatia nguvu .

Leo jumapili ya tarehe 14/10/2012 tulikuwa na ibada iliyofanyika chuoni Ruco katika ukumbi c iliyoongozwa na Mchungaji wa Usharika,Mchungaji Canon Nyagawa na vilevile tuliweza kupata nasaha zenye kujenga katika maisha ya kiroho tunapokuwa chuoni.Madaam Baby Baraka Chuma aliwashauri wanafunzi wa mwaka wa kwanza kuwa wanapokuja chuoni wasije wakaishi maisha ya kidunia (Artificial Life) badala yake  wanatakiwa kujua malengo yaliyowaleta ikiwemo kusoma kwa bidii na kuwa wawazi na wakweli kwa wazazi na chuo kwa ujumla na hii yote itafanikiwa iwapo watamcha Mungu.
Madaam Baby Baraka Chuma akitoa nasaha kwa wana CCT Ruco na  kulia ni Mchungaji Canon Nyagawa.





Wana CCT Ruco wakisikiliza kwa makini nasaha zinazotolewa na Madaam Mlezi.

Katika ibada hiyo walitambulishwa viongozi wa CCT Ruco kwa mwaka wa kwanza ili waweze kuwatambua na vilevile ilifanyika harambee ya kununua vyombo vya kwaya kwa wana CCT  iliyoendeshwa na Mchungaji wetu na viongozi walikuwa mstari wa mbele kama tunavyoowaona katika picha hapa chini.



Baada ya harambee ya vyombo mwenyekiti wa CCT Ruco aliwakaribisha mwaka wa kwanza na katibu wa CCT Ruco Bw Jackson Mustapha aliweza kuwasomea utaratibu watakaoufuata muda wote watakapokuwa chuoni ikifuatiwa na kujaza fomu za usajili kama wanachama wapya wa CCT Ruco.
Wana CCT wa mwaka wa kwanza wakisikiliza kwa makini utaratibu wa kujaza fomu za usajili.
Wana CCT wa mwaka wa kwanza wakiwa katika picha ya pamoja na mwenyekiti wa CCT baada ya ibada


2 comments:

  1. kaka tunashkru sana kuwa unafanya kazi nzuri sana ili tuomba sana uonyeshe matukio mengi maana yapo matukio mengi sanaaaaaaaa matukio ya cct ruco

    ReplyDelete
  2. HONGERENI, LAKINI Jamani mbona hii blog ina matukio ya zamani sana, matukio tunayasikia na mengine kuyaon mbona hamtyuwekei ili kuwa up todate zaidi ?

    ReplyDelete