Wednesday, May 29, 2013

Mahafali ya CCTRUCO yapendeza

Tunamshukuru Mungu wa mbingu na nchi kwa kutuwezesha na kutufanikisha kufanya mahafali yetu kwa wahitimu mwaka 2013 iliyofanyika tarehe 26 Mei 2013,mahafali ilifanyika vizuri sana,hii ni kwa sababu na kujipanga pamoja na kuwa na moyo wa ushirikiano  kwa wana cct wote katika kuindaa mahafali hiyo chini ya uongozi mzuri wenye ushirikiano wa M/kiti wa CCT-RUCO ndugu Laurence Mwamakula.

Mahafali hiyo imesisimua kwa namna ya kipekee sana kwani wahitimu pamoja na uongozi waliamua kufanya mahafali hii kipekee kwa ushirikiano kabisa kama ilivyo kawaida na desturi ya wana cct-ruco, Takribani ya wahitimu 200 waliofanyiwa mahafali siku hiyo,idadi hiyo inajumuisha  wanafunzi wanaosoma kitivo cha Elimu,Mawasiliano na Teknolojia,Sheria,Biashara,Phamarsia pamoja na wataalam wa Maabara.

Wageni walioarikwa katika Mahafali hii ni; mgeni rasmi ndugu Engineer Ramo Makani,Baba Askofu Dr.Joseph Nghambi Mgomi, wageni wenyeji, waimbaji, viongozi mbalimbali,wachungaji wa makanisa mbalimbali yaliyo chini cct,viongozi wa cct kutoka Vyuo mbalimbalia kama vile Cct Mkwawa,Cct Tumaini na vingine,pamoja wanafunzi wenyeji kutoka madhehebu mbalimbali.Jumla ya idadi ya watu waliohudhuria siku hiyo ni zaidi ya mia sita(600).
Wahitimu nao walikuwa wamejipanga wakipendeza vizuri kabisa kama desturi yao ya kuwa watana shati kama wanavyoonekana katika picha.
"
Baba askofu aliwapawapa nasaha mzuri wenye kujenga kiroho kuwa waendelee kukaa ndani ya Kristo kama walivyokuwa wamekaa pindi wakimtumikia hapa cct-ruco vivyo hivyo wakaendelee kuwa watumishi wazuri na mashaidi wa Yesu Bwana wetu katika kazi zao,katika jamii na Taifa kwa ujumla
Pia Mwalimu mlezi Madam Baby Baraka Chuma ameweza kusisitiza kuwa wao ni chumvi na nguzo ya taifa la sasa na lijalo hivyo wanatakiwa wakaitumie vizuri Elimu yao pamoja na Maadili mazuri walionayo na walioyapata kipindi wanasoma hapa Chuoni kutoka kwa watumishi mbalimbali wa Mungu na walezi wao kupitia cct-ruco.


1 comment: