Saturday, May 3, 2014


WANA CCT WAPATA VIONGOZI WAPYA WAPYA WA CCT 2014/2015

Wana CCT wamepata viongozi wapya baada ya uchaguzi uliofanywa na wana CCT kufuatia viongozi waliokuwepo kumaliza muda wao. Uchaguzi ulisimamiwa na kamati makini ya uchaguzi wakisaidiana na Mchungaji wa Usharika ambaye alikuwa mshauri katika zoezi hilo. Baada ya shuguri nzuri ya uchaguzi  wajumbe walipata viongozi wapya walioingizwa hudumani kwa ajili ya utumishi wa kazi ya Bwana kwa mwaka 2014/2015. 

WAJUMBE WA KAMATI KUU

Kutoka kushoto ni Bi Magreth Mtui, Mhazini, Bi Lucy Samsoni,Katibu msaaidizi, Bw. Daudi Jacob Katibu mkuu, Bi Beatice Herman, Makamu Mwenyekiti na Bw. Josam Mabaraza- Mwenyekiti.

 Wana CCT katika ibda ya kusimika viongozi
 Viongozi wakati wa zoezi la kusimikwa

Wazee wa kaanisa wakisikiliza kwa makini maneno ya utume
Kama ilivyokawaida ya mzazi, kuwaasa watoto ni muhimu. Mchungaji akitoa neno la kuwafunda viongozi wapya kabla ya kuanza kazi. Ni ujumbe wa kutia moyo watenda kazi hawa wapya wa Bwana.
Basi endeni mkaifanye kazi ya Bwana tena kwa ukamilifu maana hambani mwa Bwana watenda kazi ni wachache na mavuno ni mengi. Ndivo waweza kuyaita maneno ya Baba Mchungaji Nyagawa
Anaonekana Bi Furaha( mwenye suti nyeupe) makamu mwenyekiti msitaafu akifuatilia kwa makini kinachojili.
Wana CCT wakifuatilia kwa makini kusimikwa kwa viongozi wao

Mgeni Rasmi akiwaingiza hudumani viongozi
Wanajuia wa CCT wakiwa katika ibada
Viongozi wote, wazee wa kanisa, viongozi wa kamati mbali mbali za CCT, viongozi wa kwaya na viongozi wa kamti kuu, wakiwa mbele tayali kuingizwa hudumani.
TUPO TAYARI KWA KAZI

WANA CCT- RUCO WAOMBOLEZA
Wana CCT walijumuika na familia ya wana RUCO pamoja na familia ya marehemu, kuomboleza msiba wa mwanajumuia mwenzao Ndugu SUBILI KILASI aliyekuwa mwanachuo kitivo cha sanaa liyefariki siku ya ijumaa ya tarehe 8/11/2013. Katika utumishi wa kanisa, marehemu Kilasi alikuwa Mwenyekiti wa Kamati ya chakula na Mwanakwaya wa kwaya ya HOPE aliyemtumikia Mungu kwa nguvu zake zote kwa njia ya uimbaji mpaka mauti yanamkuta. Hakika ni pengo kubwa lakini katika Kristo tunayo imani kuwa Mungu aliifurahia kazi yke aliyoifanya kuwahubiri watu kwa njia ya uimbaji.

 Mwili wa marehemu Kilasi ukiwa nyumbani kwao
 Jeneza lenye mwili wa marehemu Kilasi ukiwa nyumbani kwao
 Waombolezaji wakiwa wamebeba mwili wa marehemu kuelekea kwenye nyumba yake ya milele
 Safari ya mwisho ya kumpeleka marehemu kilasi kuelekea kwwenye nyumba yake ya milele
 Wana CCT pamoja na wanachuo katika safari ya kulekea makaburini
 Mwinjilisti akiongoza safari ya kuelekea makaburini kumsindikiza ndugu Kilasi kwenye makazi yake ya milele



Waombolezaji wakiweka mashada ya maua kwenye kaburi la marehemu Kilasa





No comments:

Post a Comment