Monday, May 5, 2014

UONGOZI WA CCT WASOMA MAPATO NA MATUMIZI YA ROBO MWAKA

     UONGOZI WA CCT WASOMA MAPATO NA MATUMIZI                                   YA ROBO MWAKA 

Kaika ibada ya leo( 4/5/2014) uongozi wa CCT umewassilisha taarifa ya fedha ya robo mwaka tangu mwezi (JANUARI-APRIL). Ripoti hiyo ilihusisha mapato na matumizi ya usharika kwa mwezi Januari hadi April na ilisomwa na Mwenyekiti wa CCT. Baada ya kusomwa kwa ripoti mwenyekiti alitoa nafasi kwa wana CCT kutoa maoni na kuomba ufafanuzi mahala ambapo hawakuwa wameelewa vizuri.


 SOMA SEHEMU YA TAARIFA YA RIPOTI HAPA

TAAIFA YA MAPATO NA MATUMIZI YA CCT KWA ROBO MWAKA ( JAN-APRL 2014)

Wapendwa Bwana Yesu Asifiwe

Tunapenda kumshukuru Mungu kwa kutupa uhai, na nguvu za kumtumikia kwa ajili ya utukufu wake. Pia tunapenda kuwashukuru ninyi washarika kwa namna tunavyozidi kusirikiana katika ibada na shughuli zote za CCT-RUCO. Maneno ya Mungu yanasema, "Tazama jinsi ilivyovema na kupendeza ndugu wakae pamoja kwa umoja (ZAB 133-1). 


         JUMLA YA MA PATO KWA MWEZI JANUARI-APRIL


S/NO
    CHANZO CHA MAPATO
KIASI KILICHO PATIKANA
BAKAA
         1.
SADAKA
1,717,650/=
1,717,650/=
         2.
ZAKA/ FUNGU LA KUMI
227,000/=
1,944,650/=
         3.
VYOMBO VYA MZIKI
0/=
1,944,650/=
         4.
SHUKRANI
75,500/=
2,020,150/=
         5.
JUMLA YA MAPATO
SALIO-BENKI
JUMLA KUU
2,020,150/=
        6.
940,000/=
         7.
2,960,150/=

Baada yazoezi la uwasilishwaji wa taarifa Mwenyekiti alitoa nafasi kwa wajumbe ili watoe maoni yao na waobe ufafanuzi
Aidha baada wajumbe kusomewa taarifa ya fedha Mwenyekiti alitoa nafasi kwa wana CCT kutoa maoni yao, na kuomba ufafanuzi mahala penye shaka. Wana CCT walito mmapendekezo yao na sehemu ya mapendekezo yao yalikuwa kama ifuatavyo.

i. Kwamba mtu wa mawasiliano ajitahidi kuwek taarifa kwenye          blog ya CCT mara kwa mara.

ii.Kwamba uongozi uangalie uwezekano wa kuboresha mapato ya      CCT kwa kufikilia kununua pikipiki ya biashara.

iii. Kwamba wana CCT washirikiane na uongozi wa CCT kufanya        uinjilisti wa mtu kwa mtu ama nyumba kwa nyumba ili                      kuongeza idadi ya washarika maana kanisa linaonekana linazidi        kupungua.

iv. Kwamba washarika wajitoe kumtolea Mungu ili kuliwezesha            kanisa liweze kujitegemea an kujiendesha.

AidhaMwenyekiti aliwaelezaa wana CCT kuwa Uongozi umelenga kupunguza matumizi ili kuwawezesha kufanikisha mipango yao ya kuwa na bakaa itakayosaidia uanziishwaji wa mradi wa kanisa, na kwamba uongozi umeonaa ni vema kwa kila Juma pili ya kuwepo na chombo kwa ajili ya washarika wote kumshukuru Mungu kwa mambo makuu aliyowatendea kwa wiki nzima, na kuwa kila Jumapili ya mwisho wa mwezi, kitawekwa chombo kwa ajili ya washarika kutoa fungu la Kumi.


                          MCHANGANUO WAMAPATO NA MATUMIZI KWA UJUMLA



MCHUNGAJI ATOA MAHUBILI JUU YA KUMTOLE MUNGU, FAIDA NA HASARA ZAKE

 A
Akillihubili neon katika ibada, baada ya washarika kutoa maoni, Mchungaji wa usharika alisoma neno kutoka katika vitabu vya.
                 
                         1.Malaki 3:7-8
                         2. Kumb 28:1-15
                         3. Mithali 3:9
                         4. 1Nyakati26:20
                         5. Mwanzo 1:7
                         6.  Kutoka 7
                         7. Walawi27-30
Mchungaji amewakumbusha washarika  kuzidi  kumtolea Mungu, ili waweze kuvuna baraka kutoka kwa Mungu kama maneno ya Bwana yasemvyo katika vitabu vilivyoorodheshwa hapo juu.

            MNADA WA KWAYA YA WAFANA

Katika kuonesha hamasa ya kuwa wamehamasika kumtoleaa Mungu wana CCT waliwezesha kununuliwa vitu vilivyoletwa na kwaya kwa njia ya mnada, ambapo vitu mbalimbali vilinunuliwa kwa njia ya mnada. Mnada huo ulioendeshwa kwa ustadi mkubwa ulikuwa wa mafanikio.

1 comment:

  1. Hongera kwa kutupatia taarifa. nashauri uingize majina ya viongozi wote wa CCT 2014/2015. Pia ingiza majina ya wahitimu wa mwaka 2014.

    ReplyDelete