Monday, May 18, 2015

USHIRIKA MTAKATIFU

"Nitamshukuru bwana kwa moyo wangu wote, nitayasimulia matendo yako yote ya ajabu"(Zab9:1), Uongozi wa CCT RUCU unapenda kumshukuru MUNGU kwa kuendelea kuwa nasi katika kuitenda kazi yake, ni katika ibada iliyofanyika tar.17/05/2015 hapa chuoni, ibada hii iliambatana na usomaji wa taarifa ya MAPATO na MATUMIZI ya robo mwaka yaani January-February, zaidi ya hayo kwaya ya HOPE ilipata nafasi ya kumshukuru Mungu katika kipindi chote walipokuwa katika shughuli ya shooting hatimaye kumalizika, pia ibada hili ilihusisha ushirika mtakatifu ambapo waumini walishiriki kwa umoja na kwa kunyenyekea sana.
"Mungu awabariki wale wote waliopata nafasi ya kuabudu pamoja nasi ameen!!"

Uongozi wa CCT-RUCU unapenda kuwakumbusha wanacct wote katika kujitoa kwa hali na mali katika maandalizi ya MAHALI ya wahitimu mwaka 2014/2015 ambayo itafanyika tar.24/05/2015 katika ukumbi wa mikutano hapa chuoni yaani ASSEMBLY HALL. 
"Mungu atawabariki wale wote wajitoao katika kuitenda kazi yake kwa moyo wote"  amen!!!
















No comments:

Post a Comment