Sunday, June 7, 2015

UPENDO WA THAMANI

Mwanadamu ameumbwa na mungu aishi duniani akidumisha upendo na kujali hali ya mtu mwingine kwa kumthamini ikiwa ni katika shida na raha. Uongozi wa CCT RUCU pamoja na waumini wake leo wamechukua muda wa kumkumbuka aliyekuwa mwanaCCT RUCO na mwanakwaya wa HOPE mwaka 2010-2013 marehemu VICTORIA NYASU aliyepatwa na umauti tar04/06/2015 huko mbeya,
 "bwana alitoa na bwana ametwaa jina lake libarikiwe amen!!!!" 
 kwa kushirikiana na makumi yaliyo shiriki msiba huo wanakwaya wa hope walivaa sare nyeusi katika ibada ikiwa ni ishara ya kumkumbuka mpendwa wao, zaidi kupitia mahubiri ya mchungaji NYAGAWA tumepata kujifunza upendo wa thamani kutoka kwa yesu kristo aliyetufia msalabani kwaajili ya dhambi zetu na kutusihi tuishi huku tukipendana na kuzingatia maagizo ya mungu. hakika ibada ilikuwa yenye mambo mengi mazuri ya kujifunza hasa kwa vijana wa kisasa.
"MUNGU AWABARIKI WOTE WALIOPATA NAFASI YA KUABUDU PAMOJA NASI KATIKA IBADA YA LEO NA KUWAWEZESHA KUPATA NAFASI YA KUABUDU TENA SIKU YA JUMA PILI IJAYO".














No comments:

Post a Comment