Sunday, January 31, 2016

IBADA YA KUSIMIKA VIONGOZI WAPYA WA CCT_RUCU

Tunamshukuru MUNGU kwa kufanikisha zoezi la kuwapata na kuwaingiza kazini viongozi wa CCT_RUCU mwaka 2016/2017. Kipekee tunapenda kumshukuru MUNGU kupitia mchungaji kiongozi Canon Nyagawa katika kuwasimika viongozi wapya. Ibada hii ilihusisha shukrani ya pekee pamoja na matoleo ya fungu la kumi. Pia katika ibada ya leo kulikua na ibada ya ushirika mtakatifu ambayo watu wote walishiriki.Ashukuriwe MUNGU aliyetuwezesha kuiandaa na kuisoma ripoti ya utendaji kazi iliyohusisha mapato na matumizi ya CCT kwa mwaka 2015/2016. MUNGU awabariki wote mliopata kushiriki katika ibada hii.







No comments:

Post a Comment