Sunday, March 27, 2016

IBADA YA PASAKA PAMOJA NA KUWEKA WAKFU MICROPHONE KWA AJILI YA MATUMIZI YA KANISA

YESU KRISTO AMEFUFUKA KWELI KWELI HALELUYA!!!!!!!!.......Siku ya leo tunakumbuka kufufuka kwake BWANA wetu YESU KRISTO kama ilivyoandikwa katika maandiko matakatifu  MATHAYO 28:1-20..Ibada ya leo ilikua ni ibada ya furaha na shangwe washarika walisifu na kumuabudu MUNGU aliye hai..Pamoja na hayo katika ibada ya leo kulikua na tendo la kushiriki meza ya BWANA ambapo washarika wote walishiriki..Kipekee tunamshukuru MUNGU wa mbinguni kwa kupata MIC mpya za kisasa kwa ajili ya kazi ya kanisa ambapo ziliwekwa wakfu na Mchungaji kiongozi Nyagawa..MUNGU wa mbinguni awabariki wote ambao walinyoosha mkono na kumtolea MUNGU kwa moyo mkunjufu pamoja na wote walioshiriki katika ibada hii ya leo AMEN!!!!.





No comments:

Post a Comment