Enyi watu wa mataifa yote msifuni BWANA kwa maana fadhili zake ni za milele na milele. Tunamshukuru MUNGU kwa matendo yake makuu juu ya maisha yetu ibada ya leo ameonekana kwa namna ya kipekee. Ni ibada ambayo pia iliambatana na changizo fupi kwa ajili ya uzinduzi wa Album mpya ya Hope kwaya ambao uzinduzi wake utafanyika 24/04/2016. Katika changizo hili washarika pamoja na uongozi wa CCT walishirikiana kwa pamoja kufanikisha tukio hilo katika ibada ya leo.Yafuatayo ni baadhi ya matukio ambayo yalitukia katika ibada ya leo
Mchungaji kiongozi Canon Nyagawa akihudumu katika Ibada |
Keki kwa ajili ya tukio la changizo ikiandaliwa na viongozi wa kamati ya uzinduzi |
Washarika wakisikiliza neno la BWANA |
Keki imekwisha andaliwa kwa ajili ya changizo |
Mzee wa kanisa akisoma Matangazo |
Praise and worship team wakihudumu katika Ibada |
MUNGU AISHIYE MILELE AWABARIKI WOTE WALIOSHIRIKI KATIKA IBADA KWA MATOLEO, CHANGIZO NA PIA WALIOFIKA KUIANDAA IBADA HII.
No comments:
Post a Comment