Sunday, May 8, 2016

IBADA YA KUSHIRIKI SAKRAMENTI YA MEZA YA BWANA

Kipekee tunamshukuru MUNGU wa mbinguni aliyetupa pumzi na uhai ya kuweza kutumika katika ibada ya leo na pia katika shughuli mbalimbali za kila siku. Ibada ya leo ilikua ni ya kipekee watu walisifu na kuabudu katika  viwango vingine. Pia katika ibada ya leo kulikua na maombezi na maombi maalumu kwaajili ya shida za watu mbalimbali na pia kuwaweka vijana waliotoka chuo cha St.joseph mikononi mwa MUNGU ili awapiganie katika mitihani wanayoanza kesho. Maombi hayo yaliongozwa na Mwenyekiti wa maombi ndugu Godfather alex. Sambamba na hayo lakini pia kulikua na Tendo la kushiriki meza ya BWANA ambapo washarika wote walishiriki tendo hilo...Lakini pia watu mbali mbali walijitokeza kumshukuru MUNGU katika shukrani ya pekee. Kamati iliyoandaa uzinduzi wa album ya Hope kwaya nayo pia ilimshukuru MUNGU baada ya hapo kamti hiyo ilitoa ripoti ya mapato na matumizi kama ilivyofanyika katika uzinduzi huo MUNGU awabariki wale wote ambao walishiriki katika maandalizi ya ibada na pia waliofika katika ibada hii kumwabudu MUNGU.

Mch.Canon nyagawa akisoma liturgia ya meza ya BWANA





Washarika wakishiriki meza ya BWANA





 Kamati ya uzinduzi wa album ya  Hope kwaya wakitoa shukrani ya pekee

Ripoti ya mapato na matumizi ya kamati ya uzinduzi wa kwaya ikisomwa na mwenyekiti wa kamati hiyo

Hope kwaya wakihudumu katika ibada

Praise and worship Team wakihudumu katika ibada

Mama mchungaji akimsifu MUNGU pamoja na Praise and worship team


No comments:

Post a Comment