Tunamshukuru MUNGU wa mbinguni aliyetusaidia na kutufanikisha kuwa na jumapili ya kihistoria na Baraka maishani mwetu. Kipekee jumapili ya tarehe 5/06/2016 tumemuona MUNGU kwa namna ya kipekee katika ibada hii iliyoambatana na matukio kama kipaimara ,mahafali, kushiriki meza ya BWANA pamoja kumpokea msharika aliyekata shauri kumfuata YESU. Baada ya ibada iliyofanyika Assembly Hall kulikua na tafrija ya kuwaaga vijana wa mwaka wa tatu ambapo katika sherehe hiyo tulipata wageni wengi wakiongozwa na Mgeni rasmi mheshimiwa Ritta kabati(Mbunge wa viti maalumu mkoa wa Iringa). Sambaba na hayo lakini pia tulikua na waimbaji binafsi pamoja na vikundi vyetu vya praise and worship pamoja na HOPE kwaya. Yafuatayo ni Baadhi ya matukio tu kama yalivyotukia karibu utazame na MUNGU akubariki!!!!
Mchungaji Rhoden akimpokea msharika aliyekubali kumfuata YESU |
Mchungaji nyagawa akihubiri neno la MUNGU |
Mchungaji Rhodeni akiwabariki vijana wanaopata kipaimara |
Mrs Ngulla akitoa salamu katika ibada |
Wahitimu wakishiriki meza ya BWANA |
HOPE kwaya wakihudumu katika Ibada |
Wahitimu wakiwa katika furaha na shangwe |
Wahitimu wakiwa katika furaha na Shangwe |
Maandamano ya Matalumbeta na wahitimu kuelekea ukumbini |
Mgeni Rasmi Mheshimiwa Ritta Kabati akitoa salamu pamoja na kujibu risala |
Mlezi wa CCTRUCU (Ms Baby chuma)- Akitoa salamu katika sherehe |
Mchungaji nyagawa akipokea Mchango toka kwa mgeni rasmi |
Wahitimu wakitoa zawadi kwa Mchungaji pamoja na mlezi wa CCTRUCU |
No comments:
Post a Comment